Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya SI USHUJAA KUKUBALI MAAMUZI YA ‘BOSMAN RULE’ KIRAHISI

STAND UTD NA VILABU VINGINE, SI USHUJAA KUKUBALI MAAMUZI YA ‘BOSMAN RULE’ KIRAHISI

Picha
Na Athumani Adam Mwaka 1990 mchezaji raia wa ubeligiji, Jean Marc Bosman ambaye alikuwa anachezea timu iliyokuwa daraja la kwanza nchini kwao iitwayo RFC Liege alishindwa kuhamia nchini Ufaransa kwenye klabu ya Dunkerque. Japokuwa Bosman alikuwa tayari amemaliza mkataba na klabu yake, lakini alishindwa kwenda Ufaransa sababu ikiwa ni Dunkerque kushindwa kufikia makubaliano na klabu ya awali ambayo Bozman alikuwa anacheza. Kipindi hicho cha miaka ya 90 na kabla ya hapo, timu ambayo inamtaka mchezaji hata kama amemaliza mkataba ililazimika kulipa ada ya usajili kwa timu ile ambayo mchezaji amemaliza nayo mkataba. Basi Bosman akaamua kutafuta haki yake, akaenda zake mahakama ya Ulaya kule nchini Luxembourg kufungua kesi kuhusu jambo hili. Kitu ambacho Bosman alikuwa anapigania wakati ule ilikuwa ni kuona mchezaji endapo anamaliza mkataba aweze kuhamia timu nyingine akiwa huru yaani timu anayotoka isipate chochote kwa kuwa haina mamlaka tena na mchezaji husika. Ilipofika mwaka 1995,...