Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Mheshimiwa Rais Wanaodhani Wako Juu ya Sheria ni Wengi Sana...Soma Kisa Hichi

Mheshimiwa Rais Wanaodhani Wako Juu ya Sheria ni Wengi Sana...Soma Kisa Hichi

Picha
MIAKA michache iliyopita, wakati wa Serikali ya Awamu ya Nne ambayo imeshapita, kuna jambo moja lilinishangaza sana.  Jambo hili lilimhusu Waziri wa Serikali hiyo na mlinzi wa benki. Kilichotokea ni kwamba Mheshimiwa Waziri alikwenda kwenye mashine ya kutolea fedha, maarufu kama ATM, huenda kwa ajili ya kutoa fedha.  Akiwa ndani ya kile chumba akaanza kuzungumza na simu. Akazungumza na simu kwa muda mrefu, hali iliyosababisha wateja waliokuwa wakiisubiri huduma hiyo kuanza kulalamika na kumlazimu mlinzi kumuomba Waziri awapishe wateja wengine waweze kupata huduma. Hilo halikumfurahisha Waziri yule na badala yake akaanza kumwuliza mlinzi kama anajua yeye ni nani, kwa kuwa yeye kama Waziri ana mambo mengi ya maana na alikuwa akizungumza na simu muhimu.  Kwa huyo Waziri, suala la kuzungumza kwenye chumba cha ATM na kuwanyima fursa wateja wengine kama yeye kuipata huduma waliyokuwa wakiihitaji kwa wakati, halikuwa tatizo kabisa. Sakata la Mheshimiwa Waziri na mlinzi wa b...