Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Wasio Waislamu wachaguliwa kuwa Wabunge Iran

Wasio Waislamu wachaguliwa kuwa Wabunge Iran

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetangaza majina ya wabunge waliochaguliwa kuziwakilisha dini zenye wafuasi wachache bungeni.Kwa mujibu wa matokeo rasmi yalioyotangazwa jana Jumatatu, Siamak More Sedeq ameibuka mshindi kuwa mwakilishi wa Mayahudi hapa nchini, kwa kupata kura 2,449. Esfandiyar Ekhtiyari ametangazwa mshindi wa jamii ya Wazartoshti baada ya kupata kura 3,966. Wizara ya Mambo ya Ndani ya Iran imetangaza kwamba, Younatan Betkolia amechaguliwa kuwawakilisha bungeni watu wa jamii za Assyria na Chald kwa kupata kura 2,212. Georgik Abrahamian ndiye amechaguliwa kuwawakilisha Wakristo wanaoishi kusini mwa Iran kwa kupata kura 2,290 huku Karen Khanleri akichaguliwa kuwawakilisha wafuasi wa dini za wachache wanaoishi kaskazini mwa nchi, kwa kura 8,631.Kwa mujibu wa Sura ya 12 ya Sheria za Uchaguzi, wafuasi wa dini za wachache nchini Iran wana haki zote za kiraia na kijamii ikiwemo haki ya kuwa na mwakilishi wao bungeni. Kati ya viti 290 vwa Majilisi ya Us...