Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Mume wa Aunt Ezekiel Kumnyang’anya Iyobo Mtoto Akitoka Jela...

Mume wa Aunt Ezekiel Kumnyang’anya Iyobo Mtoto Akitoka Jela...

Picha
 Imevuja! Mume wa mwigizaji mahiri wa filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel, Sunday Demonte, huenda akaachiwa huru baada ya kusota gerezani, Abu Dhabi, Falme za Kiarabu alikofungwa tangu mwaka 2014. Demonte aliyefunga ndoa ya Kiislamu na Aunt Ezekiel, Novemba 2012, alitiwa nguvuni na polisi wa Dubai akikabiliwa na makosa kadhaa, likiwemo la kuishi nchini humo bila kuwa na kibali na kuhukumiwa kifungo jela. Kwa mujibu wa chanzo chetu ambacho ni rafiki wa karibu wa mwanaume huyo, Demonte anatarajiwa kuachiwa huru katika msamaha maalum unaotolewa kabla ya kuanza kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan kila mwaka, baada ya kuonesha tabia njema katika kipindi chote akiwa gerezani. “Amebadilika sana akiwa gerezani, muda wote yeye ni mtu wa kuswali, kutokana na tabia nzuri anayoionesha, serikali ya kule imeona bora na yeye aingizwe katika kundi la watu watakaoachiwa kwa msamaha maalum mwanzoni mwa Juni kabla ya mfungo kuanza,” kilisema chanzo hicho. Chanzo chetu kilizidi kutir...