Serikali Kuendelea Kuwachukulia Hatua Waliobadili Matumizi ya Ardhi Ya Makazi kuwa ya Biashara
Serikali imesema kuwa itawachukulia hatua za kisheria wananchi waliobadili matumizi ya Ardhi ya makazi kuwa maeneo ya biashara kinyume cha sheria na kuifanya Serikali kukosa mapato stahiki ya kodi ya Ardhi. Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es salaam na Kaimu Mkuu wa Kitengo Cha Kodi toka Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bi.Rehema Kilonzi wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu mapato yaliyokusanywa kutokana na kodi ya pango la ardhi kwa mwaka fedha 2015/2016. Amesema kuwa baadhi ya wananchi katika maeneo mbalimbali nchini wameyageuza maeneo yaliyopangwa kwa ajili ya makazi ya watu kuwa maeneo ya nyumba za kulala wageni,hosteli, maeneo ya biashara jambo ambalo ni kinyume cha Sheria ya Ardhi Namba 4 ya mwaka 1999 chini ya fungu la 33. “Rai yetu kwa wananchi waliopata fursa ya kumiliki maeneo yaliyopangwa na kumilikishwa kisheria,tunawaomba walipe kodi ya Pango la ardhi kwa wakati kuepuka usumbufu wa kufi...