Ufahamu ugonjwa wa ‘Mkanda wa jeshi
MPENZI msomaji wa ukurasa huu wa afya, leo tuangalie ugonjwa unaojulikana kama mkanda wa jeshi. Tumekuwa tukishuhudia baadhi ya watu wenye ugonjwa huu wakionekana kuwa wana maambukizi ya VVU bila kuwa na uhakika wa afya zao au bila kutambua chanzo sahihi cha ugonjwa wenyewe.Hali hii imewafanya baadhi ya watu kuamini kuwa mtu mwenye ugonjwa wa mkanda wa jeshi anakuwa na ugonjwa wa UKIMWI jambo ambalo halina ukweli kwa asilimia mia moja kwani sio wote wenye ugonjwa huu wanakuwa na VVU.Ugonjwa huu kitaalamu unajulikana shingles au herpes zoster ambapo ugonjwa huu husababishwa na virusi aina ya Varicella-zoster ambao pia husababisha ugonjwa wa tetekuwanga. Ugonjwa huu wa mkanda wa jeshi huathiri ngozi ambapo huambatana na vipele na michubuko kama ya kuungua yenye kuambatana na maumivu makali.VisababishiDk Grace Chirwa kutoka Hospitali ya Temeke Dar es Salaam anasema kuwa ugonjwa huu husababishwa na virusi aina ya Varicella-zoster ambao pia husababisha ugonjwa wa tete...