Profesa Lipumba Atangaza Kurejea Kwenye Nafasi yake ya Mwenyekiti wa CUF.........Amwandikia Barua Katibu Mkuu wa Chama Hiyo Kuomba Atengue Kujiuzulu Kwake
HATIMAYE Prof. Ibrahim Lipumba, aliyekuwa Mwenyekti wa Chama cha Wananchi (CUF) ametangaza kurejea kwenye nafasi yake ya uenyekiti-taifa wa chama hicho. Amesema, anarejea kwenye nafasi hiyo baada ya muda wa kutosha alioutumia kutafakari siasa za nchini na namna demokrasia inavyokanyagwa na watawala wa nchi hii. “Nimemwandikia Katibu Mkuu (Maalim Seif Sharif Hamad) kutengua barua yangu niliyoandika 5 Agosti mwaka jana,” amesema Prof. Lipumba. Prof. Lipumba alijiuzulu nafasi yake mwaka jana kwa madai ya kutoridhishwa na uamuzi wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kumridhia Edward Lowassa kupeperusha bendera ya umoja huo kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2015 kupitia Chadema. Hata hivyo amesema, analazimika kurejea kwenye nafasi ya uenyekiti wa chama hicho taifa kutokana na kuguswa na matatizo ya demokrasia nchini. Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam amesema kuwa, amemuandikia barua Maalim Seif ili atengue uamuzi wake wa awali wa ...