Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya MNAPOSHEREHEKEA UFALME WA KARIAKOO

MNAPOSHEREHEKEA UFALME WA KARIAKOO, MZIFIKIRIE NA ZILE BILIONI 5 ZA CAF

Picha
Na Eusebius Paul Hakuna marefu yasiyo na ncha, ndiyo kauli muafaka unayoweza kuitumia ukiisindikiza kwa kushusha pumzi ndefu ili kuruhusu oblongata yako irejee katika utulivu wake wa kawaida. Hatimaye ligi kuu ya soka nchini Tanzania (bara) inaelekea ukingoni ilhali kila klabu shiriki ikiwa imekwisha tambua hatma yao pindi vipyenga vya mwisho vitakapopulizwa na waamuzi kutoka viwanja vinane tofauti majira ya saa 12 jioni ya Mei 22, Jumapili hii. Ukiachilia mbali mchuano uliobakia katika kuwania nafasi ya pili ya ligi pamoja na kuepuka kushuka daraja, tayari mabingwa wa msimu wa 2015/16 Dar Yanga Africans wamekwisha kabidhiwa ndoo yao mbele ya maelfu ya mashabiki na viongozi wa kiserikali, lakini hasa mbele ya uwepo wa familia za wachezaji wenyewe. Licha ya figisu nyingi tulizozishuhudia katika msimu huu wa ligi lakini ni dhahiri Yanga waliustahili ufalme huu na kujitwalia tiketi ya kupanda tena ndege kushiriki ligi ya Mabingwa katika msimu ujao, wakati Azam FC wakikata tiketi ya k...