Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Serikali kukosa mabilioni ya msaada toka USAID

Serikali kukosa mabilioni ya msaada toka USAID

Picha
Serikali itakosa mchango wa dawa zenye thamani ya Dola 375 milioni za Marekani (Sh787 bilioni), ambazo zimekuwa zikichangwa na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Marekani (USAID). USAID ilitoa mchango huo chini ya mradi wa kutunza na kugawanya dawa hasa za kupunguza makali ya virusi vya Ukimwi (ARV) kwa kipindi cha miaka 10 nchini. Mradi huo ambao pia umeisaidia Serikali kujenga maghala ya kuhifadhia dawa umefikia mwisho. Hata hivyo, Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsi, Wazee na Watoto, Dk Mpoki Ulisubisya alisema licha ya mradi huo kufikia ukomo na kuwa na msaada, wizara imejipanga kuhakikisha kuna uhakika wa upatikanaji wa dawa nchini. Dk Ulisubisya alisema hata bajeti ya mwaka 2016/17 ya Wizara ya Afya imetoa kipaumbele kwenye dawa. “Tunataka kuhakikisha Watanzania wanafikiwa na huduma ya dawa kote nchini,”  alisema. Dk Ulisubisya alisema kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita, USAID ilitekeleza mradi huo na wananchi zaidi ya 8,000 wamefikiwa ...