Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya HANS POPPE AWE KAIZER MOTAUNG MRADI WA BOKO

SIPENDI SIMBA IWE KAIZER CHIEFS, HANS POPPE AWE KAIZER MOTAUNG MRADI WA BOKO

Picha
Na Athumani Adam Nadhani unaifahamu Kaizer Chiefs, klabu ya mpira wa miguu yenye makazi yake jijini Johannesburg maeneo ya Soweto. Inasemekana ni klabu yenye mafanikio zaidi nchini Afrika Kusini, wana vikombe vya ndani takribani themanini tangu ilipoanzishwa mwaka 1970 na aliyekuwa mchezaji wa zamani wa Orlando Pairets, wapinzani wa Kaizer Chiefs Bw Kaizer Motaung. Kaizer Motaung aliporudi kutoka Marekani alipokuwa anacheza soka la kulipwa aliamua kuanzisha klabu ikaitwa Kaizer Chiefs maarufu kama ‘Amakhosi’. Licha ya mafanikio ya Kaizer Chiefs timu ya mchezaji wa zamani ya Leeds United ya Uingereza Lucas Radebe, lakini wamezunguka viwanja vipatavyo tisa kuchezea mashindano mbalimbali kama viwanja vyao vya nyumbani. Mwaka 2006 walianza kujenga uwanja wao wa nyumbani, uwanja ambao ungeitwa jina lao la utani yaani Amakhosi Stadium. Bajeti ya takribani rand bilioni 1.2 za Afrika Kusini ilikadiliwa kujenga uwanja wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 55,000. Uwanja ambao ungekuwa wa kias...