Uchaguzi wa Marudio Zanzibar Unaendelea Kwa AMANI na UTULIVU.......Wananchi Wameitikia na Ulinzi Umeimarishwa
Wananchi wa Zanzibar leo wanapiga kura katika uchanguzi wa marudio baada ya kufutwa kwa uchanguzi uliofanyika October 25,2025 kutokana na kasoro zilizojitokeza. Katika baadhi ya vituo wananchi wamejitokeza na zoezi linaendelea vizuri huku hali ya usalama ikiwa imeimarishwa. Katika kituo cha shule ya sekondari Muembeladu ambayo ina vituo sita,vituo vitano vinawatu 350 na kituo kimoja kina watu 91. Akizungumza na wanahabari, msimamizi wa kituo hicho amesema zoezi la upigaji kura linaendelea vizuri katika jimbo la Jangombe . Kwa upande wa kituo cha skuli ya Muembeshauri nako hali ni shwari na zoezi linaendelea vizuri ambapo katika skul hiyo vituo 11 vinatumika watu kupiga kura. Katika Jimbo la kikwajuni, zoezi linaendelea vizuri huku mwitikio wa watu ukiwa ni mkubwa. Baadhi ya wananchi waliojitokeza kupiga kura wamesema zoezi hilo limekua rahisi na la amani tofauti na taarifa zilivyokua zinasambazwa. Mkazi wa Muembeshauri aliyejitambulisha kwa jina la Hamidu Salum Haji a...