Tume ya mipango yazindua muongozo wa usimamizi wa utayarishaji miradi katika secta ya umma Tz
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango akitoa hotuba katika mkutano wa uzinduzi wa kitabu cha Mwongozo wa Usimamizi na Utayarishaji wa Miradi ya Uwekezaji katika sekta ya Umma kilichofanyika mjini Dodoma. Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kitabu cha Mwongozo wa Usimamizi na Utayarishaji wa Miradi ya Uwekezaji katika sekta ya Umma, kushoto ni Katibu tawala wa mkoa wa Dodoma bibi. Rehema Madenge na kulia ni bi Anna Kimwela kutoka Tume ya Mipango. Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango akionesha kitabu cha Mwongozo wa Usimamizi na Utayarishaji wa Miradi ya Uwekezaji katika sekta ya Umma (Public Investment Management Operational Manual), kulia ni Kaimu katibu mtendaji wa Tume ya Mipango Bibi Florence Mwanri na kushoto ni katibu tawala wa Mkoa wa Dodoma Bibi Rehema Madenge. Kaimu naibu katibu mtendaji kutoka Tume ya Mipango anayesimamia klasta ya uchumi jumla, dkt. Lorah Madete akijibu hoja zilizotolewa n...