ARGENTINA YATISHIA KUJITOA COPA AMERICA
Chama cha soka nchini Argentina (AFA) kimetishia kuitoa timu yake ya taifa nje ya mashindano ya Copa America kutokana na serikali ya nchi hiyo kuingilia masuala ya soka. Argentina ni miongoni mwa timu ambazo zinapewa nafasi kubwa ya kuibuka bingwa wa michuano hiyo itakayofanyika Marekani na June 7 wanatarajia kucheza mchezo wao wa kwanza dhidi ya mabingwa watetezi Chile kwenye mji wa Santa Clara, Califonia. Lakini ushiriki wao umeingia mashaka baada ya AFA kuingia kwenye mgogoro na serikali ya Argentina kufuatia serikali kuusimamisha uchaguzi wa rais wa chama hicho kinachosimamia soka la Argentina ambao ulipangwa kufanyika June 30 huku wakiteuliwa ma-inspectors kuchunguza tuhuma za mapato ya TV ambazo zinalikabili shirikisho hilo. Katibu mkuu wa AFA Damian Dupiellet amekiambia kituo kimoja cha redio nchini humo kwamba, bodi ya mkutano wa dharura itaamua kama timu ya taifa ya Argentina itarudishwa nyumbani kutoka Califonia ambako inaendelea na maandilizi kuelekea mashindano hayo. ...