Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Wanaodai bunge kuonyeshwa live watakiwa kuomba kwa utulivu

Wanaodai bunge kuonyeshwa live watakiwa kuomba kwa utulivu

Picha
Katibu Mkuu wa National Reconstruction Alliance (NRA), Hassan Kisabya Almas amewataka  Watanzania wanaoomba Bunge  la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuonyeshwa  kupitia matangazo ya moja kwa moja (Live) kuomba  kwa utaratibu bila kuharibu amani ya Tanzania. Aidha Katibu Mkuu wa Chama hicho, amesema  kwamba   amani iliyoko ni hazina kubwa ambayo nchi nyingine inatamani kuwa nayo. Almas aliyasema hayo jana alipokuwa akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO). “Leo hii tupo tunaopigania kutaka kuona Bunge Live, lakini yote haya ni kwa kuwa Tanzania amani tunayo, sidhani kama nchi kama Afghastan siku watakayoamua kuonyesha Bunge Live kwa mwaka mzima, kwa saa 24 kama wataweza kukaa kuangalia Bunge hilo, hivyo basi wale wanaotaka hayo, kwanza tudumishe amani  yetu,”  alisema Almas. Almas alieleza kuwa, amani ya Tanzania ni zaidi ya dhahabu ambayo Tanzania inajivunia hivyo ni lazima Watanzan...