Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya bosi wake".- kasema Zitto Kabwe

Waziri Kitwanga sio 'size yangu'.....Size yangu mimi ni Rais Magufuli, bosi wake".- kasema Zitto Kabwe

Picha
Kiongozi Mkuuwa Chama cha Allience for Change and Transparency(ACT), Zitto Zuberi Kabwe, ameibuka na kujibu mashambulizi juu ya taarifa zinazoenezwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga kupitia Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (CCM) za kumhujumu Rais Dk. Magufuli katika utendaji wake. Kiongozi huyo amesema anaushahidi wa moja kwa moja juu ya vitendo vinavyofanywa na Waziri huyo katika kueneza propaganda zinazolenga kuiyumbisha Serikali .   “Nina ushahidi usio na mashaka wa Kitwanga kupanga Vijana wanaojiita wa UVCCM kufanya mikutano na Waandishi wa Habari na anawalipa fedha kufanya hivyo, nataka ieleweke wazi kuwa nina muunga mkono Rais katika kazi ya kusafisha Nchi … nitakuwa mtu wa ajabu nisipo muunga mkono katika vita dhidi ya ufisadi”  amesema Zitto Kabwe.   Zitto amemtaka Waziri Kitwanga kuepuka siasa za porojo na kusema waziri huyo si ‘size’ yake na hana mpango wa kumtoa katika nafasi ya uwaziri hivyo aache kulalamika na kueneza uzushi....