Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Tundu Lissu Amshauri Rais Magufuli Atumbue Washauri wake

Tundu Lissu Amshauri Rais Magufuli Atumbue Washauri wake

Picha
RAIS John Magufuli ametakiwa kutumbua majipu ya wanasheria walioshindwa kumshauri kufuata sheria ya kukasimisha mamlaka ya kiuwaziri kwa mawaziri walioteuliwa miezi sita iliyopita.   Tundu Lissu amesema hayo Dodoma wakati akitoa maoni kuhusu Mpango na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha ya wizara ya Sheria na Katiba kwa mwaka wa fedha wa 2016/2017, Bungeni mjini Dodoma. “Kwa kuangalia mifano ya matangazo mbalimbali ambayo yametolewa na watangulizi wa Rais Magufuli tangu sheria ya utekelezwaji wa majukumu ya kiuwaziri ilipotungwa mwaka 1980, hata mwanafunzi wa sheria wa mwaka wa kwanza angeweza kumtengenezea draft ya Tangazo la aina hiyo,”  amesema Lissu. Ameongeza  “iweje watu wenye Shahada za uzamivu na uzamili katika sheria washindwe kufanya hivyo kwa karibu ya nusu mwaka tangu wateuliwe? Kama ni majipu ya kutumbuliwa na Magufuli, basi wasomi hawa wa sheria ni majipu na wanastahili kutumbuliwa.” “Kwa sababu Rais Magufuli sio mwa...