TWEET YA KWANZA YA GUNDOGAN BAADA YA KUSAJILIWA MANCHESTER CITY
Manchester City wamekamilisha usajili wa kwanza baada ya kumsajili kiungo wa Borussia Dortmund Ilkay Gundogan kwa mkataba wa miaka minne. Licha ya kutowekwa wazi kwa gharama za usajili wa kiungi huyo, inaripotiwa kuwa amesajili kwa ada ya zaidi ya paundi milioni 20. Huo unakuwa usajili wa kwanza kufanywa na Pep Guardiola ambaye ndiye kocha mpya wa Manchester City. “Ninayo furaha kubwa sana kusajiliwa kunako klabu hii ya Manchester City”, Gundogan aliiambia tovuti ya Manchester City. “Nilivyojua kwamba City wananihitaji nilitamani sana kuja hapa na hakika mambo yamekwenda kama nilivyotarajia”. “Sitasahau kipindi chote nilichokuwa na Borussia Dortmund na ningependa kuishukuru klabu na mashabiki kwa sapoti yao kwa kipindi chote cha miaka mitani niliyokuwa klabuni pale”. “Wao ndio walionifunguliwa njia ya kuwa kama nilivyo, na kuwa mchezaji bora kutokana na imani na uvumilivu wao mkubwa kwangu Sasa naenda kukutana na changamoto mpya ambayo ni...