SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 2 Juni 2016

T media news

TWEET YA KWANZA YA GUNDOGAN BAADA YA KUSAJILIWA MANCHESTER CITY

Manchester City wamekamilisha usajili wa kwanza baada ya kumsajili kiungo wa Borussia Dortmund Ilkay Gundogan kwa mkataba wa miaka minne.

Licha ya kutowekwa wazi kwa gharama za usajili wa kiungi huyo, inaripotiwa kuwa amesajili kwa ada ya zaidi ya paundi milioni 20. Huo unakuwa usajili wa kwanza kufanywa na Pep Guardiola ambaye ndiye kocha mpya wa Manchester City.

“Ninayo furaha kubwa sana kusajiliwa kunako klabu hii ya Manchester City”, Gundogan aliiambia tovuti ya Manchester City. “Nilivyojua kwamba City wananihitaji nilitamani sana kuja hapa na hakika mambo yamekwenda kama nilivyotarajia”.

“Sitasahau kipindi chote nilichokuwa na Borussia Dortmund na ningependa kuishukuru klabu na mashabiki kwa sapoti yao kwa kipindi chote cha miaka mitani niliyokuwa klabuni pale”.

“Wao ndio walionifunguliwa njia ya kuwa kama nilivyo, na kuwa mchezaji bora kutokana na imani na uvumilivu wao mkubwa kwangu

Sasa naenda kukutana na changamoto mpya ambayo ni kujitolea ili kuleta mafanikio kwa Manchester City. Fursa ya kufanya kazi na kocha aina ya Pep Guardiola ni adhimu mno kwangu, na nimefurahishwa sana kuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa chini yake.

“Nawaahidi mashabiki wa City kujitolea kwa kila kitu kuisaidia timu kushinda mataji mengi hapa England na Ulaya pia (Champions League). Hizi ni nyakati za kuvutia sana.”

“Naamini nina miaka kadhaa ya mafanikio mbele na nadhani tunaweza pia kufanikiwa mambo mengi sana kwa pamoja. Nasubiri kwa hamu kubwa msimu mpya nikiwa katika klabu mpya.

Gundogan ni windo la kwanza la Manchester City kukamilika, wengine wanaowaniwa kwa karibu na City ni beki wa Athletic Bilbao Aymeric Laporte na beki wa Everton John Stones.

Wengine ni kiungi wa Real Madrid Mjerumani Toni Kroos Paul Pogba wa Juventus.

Gundogan anakuwa mchezaji wa pili muhimu Dortmund kuondoka baada ya beki wa kati Mats Hummels kusajiliwa na Bayern Munich.

Gundogan ameacha ujumbe huu kwa Borussia Dortmund

Hi guys,

“Baada ya miaka kadhaa ya mafanikio na Dortmund kuisha. Tulisherehekea ushind mwingi na kusimama pamoja tuliopkuwa tukifungwa.

Shukrani za dhati ziwafikie makoacha wa BVB Jurgen Klopp na Thomas Tuchel. Niliishi nao vizuri na kunifanya niwe mchezaji wa kutegemewa timu ya taifa ya Ujerumani. Nawashukuru sana waajiri wangu, wachezaji wenzangu na kwa mashabiki wote walikuwa nyuma yangu.

Sababu kuwa ya uhamisho wangu ni uwepo wa fursa adhimu ya kuungana na Pep Guardiola na klabu ya Manchester City. Guardiola aliniomba kujiunga naye na kutokana na mbinu zake za ufundishaji nimeshawishika. Naamini hii ni hatua muafaka kwangu kwa sasa. Chini ya uongozi wake nataka kuboresha zaidi ujuzi wangu wa kucheza soka.

Ninayo furaha kubwa licha ya majeraha niliyo nayo lakini nimetimiza azma yangu ya kutoondoka Dortmund kama mchezaji huru.

Nawatakia maisha mema BVB kwa siku za baadaye na nitajitahidi kurejea katika hali yangu ya kawaida kwa mara nyingine tena haraka iwezekanavyo”.