SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 2 Juni 2016

T media news

MFANYAKAZI WA UBALOZI WA TANZANIA UN AZIDI KUMCHAFUA BABA WA WATOTO WAKE SASA AJIUNGA NA MANGE KIMAMBI LIVE!!

NA MWANDISHI WETU.........Blogu ya Wananchi jana kwa mara nyingine tena ilishuhudia The King Of All Bongo Social Media
akichafuliwa kwenye Instagram na MangeKimambi kufikia mpaka kuweka copy ya Passport ya The King kwenye mshambulizi ambayo Mange alidai kwamba hata Shamba na Nyumba ya Le Mutuz kule Kinyerezi ni mali ya Neema na Wazazi zake sio la Le Mutuz. Mange alizidi kudai kwamba Le Mutuz alikuwa hajasoma kabisa ila alikuwa ni Dreva tu wa Malori ya Kinyesi tu huko USA. Mange alienda mbali mpaka kudai kwamba Le Mutuz ambaye ni Mmiliki wa Blog hii ni binadam anayeishi kwa kupewa pewa na kuomba omba kwa watu hana maisha kabisa hata nyumba anayoishi hapa Bongo sio yake amepewa tu na Juma na hata gari pia sio lake amepewa na Juma au Majizo. 

 Blogu ya Wananchi kama kawaida ikaingia kazini kufanya utafiti wa kina wa suala zima la Le Mutuz kushambuliwa vile mpaka kubandikwa copy ya Passport yake na haya ndio matokeo ya utafiti wa Blogu hii:- Ni kwamba miezi kadhaa iliyopita ex huyo wa Le Mutuz alimuomba "MREKEBISHATABIA" huko Instagram kumshambulia Baba huyo wa watoto wake 2 kwa maneno mengi makali sana mpaka kutundika picha za watoto wao. Mwanamama huyo hakuridhika akaanzisha mashambulizi mazito sana huko Jamiiforums akitumia majina ya bandia lakini maneno yale yale kama ya Mange jana. 

Blogu ya Wananchi ilipomuuliza mtu wa karibu sana na Mange alisema "NI EX WA LE MUTUZ NDIYE ALIYE KUWA AKIMPA MANGE JANA HABARI ZOTE AKIDAI KWAMBA ANATAKA KUMKOMOA NA KWAMBA ANALIPIZA KISASI CHA KUMUACHA NA KURUDI NYUMBANI KUMUACHA NA WATOTO" 

Baada ya kupata habari zote hizi Blogu ya Wananchi ikaanza kumtafuta The King Le Mutuz na kumkuta Masaki at Vodacomshop akiwa kwenye shooting ya Vodacom 4G promotions na tulipomuuliza kulikoni na mambo ya kushambuliwa kwake Instagram na Blogu inajua tayari kwamba ni ex wake ndiye aliye nyuma ya mashambulizi Le Mutuz Nation alijibu ifuatavyo:.

."Ni miaka 5 sasa toka tulipoachana kisheria tena kwa juhudi zake yeye mwenyewe my ex, nilijaribu kila njia na mashahidi wapo kumbembeleza kurudi kwenye Ndoa aligoma katakata kwamba hataki nikaamua kuheshimu uamuzi wake. Sasa since then huwa nashangaaa sana haishi kunifuata fuata kila mahali yaani mtu anaishi USA lakini haishi kufuatilia maisha yangu Tanzania mimi sijawahi na nilishasahau. Hapo nyuma nilisikia aliolewa kwa siri na Mume wa Mtu lakini ghafla nikashangaa yeye na huyo mume wake wakinishambulia sana Jamiiforums. So now ananihakikishia kwamba alikuwa anatingisha kibiriti amekikuta kimejaa sasa anahangaika sana kwenye mitandao maana kwa akili yake ndogo anadhani ninaweza kuogopa matusi yake na kumrudia, nimrudie Mwanamke aliyeolewa tayari na mume wa mtu? Inawezekana vipi? Ninamuombea kwa Mungu kwamba Mange atamsaidia kupata amani anayoitafuta sana kwenye Social Media, mimi I get paid kufanya kazi za Social Media so ukinichafua kwenye Instagram unaniongezea sana followers like toka jana na leo wameongezeka followers 3,000. I mean ninampa pole sana anazidi kunihakikishia kwamba hana maisha na ananihitaji na SITAMRUDIA TENA IN MY LIFE WALA HATA SITAKI KUMUONA USONI MWANGU" cause ni binadam mwenye spirit ya ajabu sana na hana shukrani maana angekuwa nayo basi angeniheshimu kwamba nilimtunza kwa miaka 5 akiwa hafanyi kazi, akarudishwa on deportation nikapigana mpaka akarudi tena USA kitu ambacho ni impossible, now hata kama nia yake ni kunichafua basi angetumia UKWELI NA FACTS kuliko kusema uongo like Nyumba na Shamba langu ni vyake na huku anajua mimi ndiye mwenyewe na nina documents zote za Nyumba na Shamba. Ninakuomba sana Bwana Muandhishi mfikishie ujumbe kwamba mimi binasfi nilishamfuta kwenye maisha yangu ndio maana ya Divorce na aliyeyataka ni yeye mwenyewe sasa analilia nini hasa? Mpeni pole sana muambieni badala ya kupoteza muda wake na kina Mange amrudie Mungu wake amsamehe na amsaidie kupata Mume bora kuliko mimi maana kwa kweli amehangaika sana na mitandao, as for me maisha yangu yanasonga mbele hayawezi kurudishwa na kelele za mitandaoni"