Faida Za Kujua Kile Unachokitaka Katika Maisha Yako
Kimsingi kila mwanadamu anapenda kuwa na maisha mazuri siku zote, hakuna hata mmoja ambaye anapenda kuishi katika maisha ambayo sio mazuri hata siku moja. Baadhi wa watu hawa hasa ya wale ambao hawajafanikiwa ukiwauliza kile ambacho wanakihitaji, wengi wao hutoa majibu ya ujumla kwamba nataka kuwa mfanyabiashara, nataka kusoma , nataka kujenga nyumba na vitu vingine vingi ambavyo mwanadamu huyu anataka kuwa au kuvifanya kwa hapo baadae. Lakini ukweli ni kwamba kusema hayo huwa tunakosea kwa sababu huwa tunayoongelea kwa mapana sana, hapa namaanisha ya kwamba lengo lako la kesho lazima liwe maalaumu. Kwa mfano usiseme unataka kuwa mbanyabishara na kuishia hapo tu, bali ni lazima uainishe ni aina gani ya biahara unayotaka kuja kuifanya na utie nia ya kweli juu ya biashara hiyo. Kwa mfano unaweza kupanga malengo yako ya hapo baadae unataka kuwa mfanyabiashara wa viatu, nguo za kiume, kike au viatu. Hata kama unataka kujenga nyumba katika maono yako lazima u...