Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Marais Duniani Wavutiwa na Vita ya Ufisadi Tanzania

Marais Duniani Wavutiwa na Vita ya Ufisadi Tanzania

Picha
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema viongozi wakuu wa nchi na washiriki wa Mkutano wa Kimataifa wa Kupambana na Rushwa, wamevutiwa na jitihada ambazo Tanzania imezichukua kukabiliana na janga hilo. Alitoa kauli hiyo jana wakati akitoa ufafanuzi kuhusu ushiriki wake kwenye mkutano wa siku moja wa wakuu wa nchi, ulioitishwakujadili suala la kupambana na rushwa duniani uliofanyika Lancaster House, jijini London, Uingereza. Waziri Mkuu alisema katika kikao cha kwanza, kilichohudhuriwa na wakuu wa nchi na viongozi wa kitaifa wapatao 20, alipata fursa ya kuelezea jinsi Tanzania ilivyoweza kupambana na rushwa kwa kuzingatia vigezo vikuu vinne. Waziri Mkuu alivitaja vigezo hivyo kuwa ni kufanya marekebisho ya baadhi ya sheria zinazohusu masuala ya rushwa; uanzishwaji wa mahakama maalum ya mafisadi ambayo inatarajiwa kuanza kazi Julai, mwaka huu; mikakati ya udhibiti wa fedha za miradi ya wananchi na utaratibu wa kubaini wala rushwa kwa kushirikisha jamii ikiwemo kutunza siri za watoa taa...