MWANADADA DAYNA NYANGE ATOA SABABU ZA YEYE KUKATAA KUOLEWA.
Msanii Dayna Nyange mwezi uliopita alihudhuria ndoa ya mshkaji wake Roma ilifanyika mjini Tanga, lakini pia mwezi uliopita kuna picha yake ilisambaa anaonekana ametupia shela la harusi yupo na mwanaume flani, akiizungumzia picha hiyo alisema kuwa picha ile ilipigwa kwenye maonyesho ya mavazi, je ana mtazamo gani kuhusu ishu za kufunga pingu za maisha. ‘’Kiukweli kabisa kuna wakati natamani niwe kwenye mahusiano natamani niwe naamka na mume wangu,naenda sehemu Fulani lakini najua nimemuacha mume wangu,yaani niwe mwanamke ambaye nina mume wangu,lakini kwa mazingira yetu ya sasa hivi yanatuwia vigumu sana kuamua au kuingia kwenye mahusiano hayo kwa sababu kadhaa yawezekana vijana tumekuwa na tamaa nyingi au watu wamekuwa waoga wa maisha wanajikuta wamekuwa waoga kwenye mahusiano ya ndoa’’ Alisema Dyna. ‘’Kuna wanawake pia siku hizi wamekuwa wakijirahisisha sana uko na mwanaume umekutana nae mwezi mmoja unataka akuoe, unawezakukuta mwanaume anataka ku...