Lipumba Azidi Kuitesa CUF
Wanachama wa Chama cha Wananchi (CUF), wameanza kushikana uchawi, huku viongozi wakitakiwa kutoa maelezo ya kwanini wameshindwa kujadili hatua ya kujiuzulu kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba. Pamoja na hali hiyo, wanachama hao wamemtaka Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad kutambua kuwa ana wajibu wa kuwasiliana na Profesa Lipumba ili arejee katika nafasi yake ya zamani kwa mujibu wa katiba ya chama hicho. Hayo yamesemwa Dar es Salaam jana, wakati wa kongamano lililoandaliwa na Kata ya Makurumla Manispaa ya Kinondoni, ambapo mmoja wa wana CUF Mohamed Mgomvi, alisema anashangazwa na hatua ya kikao cha Baraza Kuu kushindwa kujadili barua ya kujiuzulu Profesa Lipumba. Alisema CUF kwa upande wa Bara, imebaki haina mtu madhubuti ambaye anaweza kukiendesha kama alivyokuwa kiongozi huyo. “Ninashangaa hapa mzee Wandwi (Mustafa), kama Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa chama unashindwa kusema ukweli. Leo hii (jana) CUF imebaki...