Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Ofisi 5 za CUF Zachomwa Moto Zanzibar

Ofisi 5 za CUF Zachomwa Moto Zanzibar

Picha
HALI ya kisiasa visiwani Zanzibar, inazidi kuwa tete huku siasa za visasi, chuki na uhasama zikionekana kurejea kwa kasi. Hali hiyo imejitokeza baada ya ofisi za matawi matano ya Chama cha Wananchi (CUF) zilizopo Pemba na moja  Unguja kuchomwa moto na watu wasiojulikana. Matukio ya kuchomwa moto kwa ofisi hizo yamekuja siku mbili baada ya watu wasiojulikana kuchoma moto maskani ya CCM ya Sauti ya Kisonge iliyopo mjini Unguja. Hata hivyo Jeshi la Polisi visiwani humo limetangaza kufanya uchunguzi wa kina ili kuwabaini watu waliohusika na matukio hayo. Uchomaji huo ulifanyika usiku wa kuamkia jana saa 8 usiku, ambapo watu hao walichoma moto na kuteketeza nyaraka za chama hicho. Matawi yaliyochomwa moto ni Kilimahewa mjini Unguja Wilaya ya Magharibi, Mkanyageni, Kiwapwa, Kiuyu Minungwini, Wingwi na Kinowe yote ya Kisiwani Pemba. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba, Hassan Nassir, amethibitisha kutokeo kwa matukio hayo. Amesema kutokana na hali hiyo tayari ameagiza askari...