Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Iran: Ulaya itoe ushirikiano katika kupambana na ugaidi na utekelezaji wa JCPOA

Iran: Ulaya itoe ushirikiano katika kupambana na ugaidi na utekelezaji wa JCPOA

Picha
Rais Hassan Rouhani ameutaka Umoja wa Ulaya utoe ushirikiano katika mapambano dhidi ya ugaidi na kusisitizia ulazima wa kutekelezwa ipasavyo makubaliano ya nyuklia (JCPOA). Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametoa wito huo leo katika mazungumzo na Rais wa Baraza la Seneti la Ubelgiji Bi Christine Defraigne ambaye yuko safarini hapa nchini. Rais Rouhani ameashiria mchango chanya wa Umoja wa Ulaya katika makubaliano ya nyuklia baina ya Iran na nchi zinazounda kundi la 5+1 na kueleza kwamba: makubaliano ya nyuklia ni mwanzo tu wa safari na si mwisho wake; na kitu pekee cha kuifanya mihimili ya makubaliano hayo iwe imara zaidi ni kutekelezwa kwa wakati na kama inavyopasa makubaliano na ahadi zilizotolewa. Rais Rouhani amebainisha kuwa ugaidi ni tatizo kubwa na sugu linaloukabili ulimwengu; na mbali na kubainisha sababu na chanzo chake amesisitiza kuwa pamoja na sababu za kiuchumi na kiutamaduni kama umasikini, ujinga, ubaguzi na kukata tamaa vijana juu ya mustakabali, lakini malalam...