Elimu kidato cha 5&6 Kigoma bure - Zitto Kabwe
Meya wa Manispaa ya Kigoma Ujiji Hussein J Ruhava ametangaza kutoa elimu bure kwa manispaa hiyo kwa kidato cha tano na sita, na gharama zake zitalipwa kutokana na mapato yanayotokana na minara ya simu katika manispaa hiyo. Taarifa hiyo imetolewa na mbunge wa jimbo la Kigoma Mjini Mh. Zitto Kabwe kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, na kueleza kuwa jambo hilo limeshapitishwa kwenye bajeti ya halmashauri ya manispaa. "Meya wa Manispaa ya Kigoma Ujiji ametangaza rasmi kwamba elimu ya kidato cha tano na cha sita katika manispaa itakuwa bila malipo. Manispaa itafidia mapato ya ada hizo kwenye mashule kupitia makusanyo yake ya ndani yanayotokana na tozo za minara ya simu", aliandika Zitto Kabwe. Pamoja na hayo mbunge huyo ametoa taarifa kuwa Meya huyo amekataa kununuliwa gari ya Tshs milioni 150, na kuelekeza fedha hizo kwenda kwenye matumizi ya maendeleo na haswa miundombinu ya mji. Pia Mh. Zitto Kabwe amesema kuwa serikali za mitaa zina changamoto kubwa katika kukusany...