Kilio Kwa watumia M-pesa, Tigo Pesa , Airtel Money na Wale wa Kwenye ATM.......Kila ukituma 1000/- utakatwa kodi 280/-
Wachambuzi na wadau mbalimbali wametoa maoni yao kuhusu Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2016/17, huku watumiaji wa huduma za fedha kwa njia ya simu wakikumbwa na maumivu wa kodi. Hiyo ni siku moja baada ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango kuwasilisha Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 20116/17. Pamoja na mambo mengine, bajeti hiyo inapendekeza kuongeza ushuru wa vinywaji baridi, maji ya juisi, vinywaji vikali, bia na sigara. Pia itawagusa watumiaji wa M-pesa, Tigopesa, Airtel Money, Ezypesa kwa kukatwa Sh 280 kwa kila Sh 1000 watakayotuma. Jana Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT-Wazalendo), alisema hatua hiyo ya Serikali kuendelea kutafuta kodi kwa kuzidi kuwaumiza wananchi inakwenda kinyume na matarajio ya Watanzania wengi. Alisema katika bajeti hiyo ya Serikali na ukusanyaji wa mapato yake, katika kila Sh 1000 itakayokatwa kwa huduma kwenye ATM kuanzia Julai Mosi mwaka huu, Sh 280 zitachukuliwa na TRA. Zitto alisema hali hiyo pia i...