Polisi Zanzibar Kuwahoji Watu 34 Wanaotumia Lugha ya Matusi Katika Mitandao ya Kijamii
JESHI la Polisi Zanzibar limetoa tahadhari kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii ambao wanaitumia kwa kuwatukana viongozi wa kitaifa, huku likiwa na orodha ya watu 34 ambao wanatarajiwa kuhojiwa zaidi kutokana na matumizi mabaya ya mitandao hiyo. Kauli hiyo imetolewa juzi na Naibu Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai Zanzibar (DCI), Salum Msangi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Makao Makuu ya Polisi Zanzibar. Alisema hivi sasa baadhi ya watu wanaitumia mitandao hiyo kinyume na maadili jambo ambalo linaweza kusababisha chuki na uhasama na kwamba ni kinyume na maadili ya wananchi wa Unguja na Pemba. Msangi alisema jeshi hilo linakusudia kuwahoji watu 34 wanaotumia mitandao hiyo ya kijamii kwa kuhamasisha vurugu pamoja na kutoa lugha za matusi kwa viongozi wa Zanzibar, jambo ambalo ni kinyume na sheria pamoja na utamaduni wa wananchi wa Zanzibar. Alisema mara baada ya kufutwa kwa uchaguzi Mkuu wa Zanzibar uliofanyika Oktoba 25, mwaka jana, kumejitokeza baadhi ya watu na vi...