Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Maalim Seif Kikaangoni LEO.....Polisi Wamtaka Aripoti Makao Makuu ya Polisi Kwa Ajili ya Kuhojiwa

Maalim Seif Kikaangoni LEO.....Polisi Wamtaka Aripoti Makao Makuu ya Polisi Kwa Ajili ya Kuhojiwa

Picha
Baada ya Jeshi la Polisi Zanzibar kuahirisha kumhoji Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, hatimaye hatua hiyo sasa imeelekea kutekelezwa. Taarifa rasmi ya jeshi hilo visiwani Zanzibar, imemtaka Maalim Seif afike katika Ofisi za Makao Makuu ya Polisi, Ziwani mjini hapa leo saa 4.00 asubuhi. Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Uhusiano kwa Umma wa CUF, Salim Bimani alithibitisha Maalim Seif kupokea barua hiyo jana wakati akiwa njiani kuelekea Dunga, Wilaya ya Kati Unguja, akiendelea na ziara yake katika majimbo ya Unguja. “Ni kweli Maalim amepokea taarifa hiyo na ametakiwa afike Ziwani (mjini hapa) kesho (leo) saa nne asubuhi,”  alisema Bimani  Bimani aliongeza kuwa hatua hiyo ya sasa imekuja baada ya jeshi hilo kuahirisha hatua ya wito wa kumhoji Maalim Seif, Ijumaa iliyopita. Barua hiyo ya kuahirisha iliyosainiwa  na Msangi kwa niaba ya Kamishna wa Polisi Zanzibar Mei 26, yenye kumbukumbu namba PHQ/ Z/C.5/4/4/TEMP/34 kwenda kwa...