AZAM FC ‘ITAWAPOTEZA’ ZAIDI SIMBA SC, YOTE HAYA YAMEANZIA HAPA… (Sehemu ya mwisho)
Na Baraka Mbolembole SIMBA SC itakuwaje masikini wakati ni taasisi kubwa na ya kale sana iliyokuwapo hata kabla ya Tanganyika kupata uhuru (1961), kisha kuzaliwa kwa Tanzania (1964)? Ngoja nikupe mfano mmoja hai, Kabla ya serikali ya awamu ya tano chini ya rais John Pombe Magufuli raia wengi wa Tanzania waliaminishwa kwamba nchi hii ni masikini sana na haiwezi kujiendesha kiuchumi bila kutegemea misaada ya mataifa makubwa duniani. Jambo ambalo kwa mtu aliyesoma na kuelewa vizuri somo la maarifa daima alikuwa akipinga. Muda mfupi wa serikali ya Magufuli madarakani nchi imejikusanyia mapato mengi baada ya kuwekwa kwa mkakati wa kudhibiti mapato ya serikali yaliyokuwa yakipotea-ama kwa walafi wachache, ama kwa wakwepaji wa kodi. Rais Magufuli anasifiwa na kila mtu hivi sasa kutokana na uwezo wake wa kuwabaini ‘wahujumu uchumi’ na kuwachukulia maamuzi. Ameyaonesha mataifa makubwa kwamba Tanzania inaweza kujiendesha yenyewe kiuchumi kwa kutegemea rasilimali zake, na vyanzo ...