Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Taarifa Fupi Kuhusu Ziara Ya Rais Wa Vietnam Nchini Tanzania Tarehe 9-10 Machi 2016

Taarifa Fupi Kuhusu Ziara Ya Rais Wa Vietnam Nchini Tanzania Tarehe 9-10 Machi 2016

Picha
Utangulizi Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti ya Vietnam Mheshimiwa Truong Tan Sang anatarajiwa kufanya ziara rasmi nchini tarehe 9 Machi 2016. Madhumuni ya  ziara hiyo ni kukuza uhusiano baina ya Vietnam na Tanzania mbao umedumu kwa zaidi ya miaka hamsini tangu kuanzishwa kwake pamoja ‎Kufungua maeneo mapya ya Ushirikiano wa kiuchumi baina ya Tanzania na Vietnam. Hii ni ziara ya kwanza ya kiongozi huyo Barani Afrika tangu aingie madarakani mwaka 2011, ambapo nchi nyingine anayotarajiwa kutembelea ni Mozambique. Rais Truong anatarajiwa kufuatana na mke wake Bi Mai Thi Hahn, mawaziri 4 wanaoshughulika na sekta za  Kilimo, Mawasiliano Uwekezaji, Afya,Viwanda na Biashara.  Aidha mgeni huyo atafuatana na ujumbe wa wafanyabiashara 30 kutoka Vietnam. Shughuli za msingi zitakazofanyika kwenye ziara Wakati wa ziara hiyo Rais Truong Tang San atafanya mazungumzo rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. John Pombe Joseph Magufuli Ikulu jijini Dar-es-Salaam...