Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Makamu wa Rais: Upinzani Kuna watu makini Wanaoweza Kuikabili Serikali

Makamu wa Rais: Upinzani Kuna watu makini Wanaoweza Kuikabili Serikali

Picha
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameonyesha kukerwa na vitendo vya wabunge wa CCM kurusha vijembe na kuutaka Umoja wa Wanawake (UWT) kuwaandalia mafunzo ili waweze kukabiliana na wapinzani ambao alisema wana watu makini na werevu kuweza kukabiliana na Serikali. Samia, ambaye pia aliweka bayana kuwa chama hicho tawala kilikumbana na upinzani mkali kwenye Uchaguzi Mkuu uliopita, alitoa kauli hiyo jana wakati akifungua semina ya wabunge, madiwani na viongozi wa CCM wa Mkoa wa Dodoma na baadaye kwenye kikao cha UWT. Akiwa katika mkutano wa Baraza la UWT, Samia aliwataka viongozi wa jumuiya hiyo kutoa mafunzo maalumu kwa wabunge wapya ili waweze kupambana na wapinzani. Alihoji ni mambo gani wanayofundishwa wabunge hao wanawake katika kutimiza wajibu wao ndani ya Bunge. “Tunawafundisha nini ama (tunawafundisha) wakajibu vijembe tu, au wakaseme nini kama wabunge waliotoka UWT?”  alihoji. Samia amesema hayo wakati maneno ya kashfa na...