Jinsi ya Kupunguza Uzito wa Mwili/Unene Kwa Kutumia Saladi
Ulaji saladi ya spinachi, matunda ya apple na parachichi unaweza kumsaidia mtu kuwa na uzito unaotakiwa kiafya. Kabla mtu hajaanza kula mlo wake wa asubuhi, mchana au usiku anashauriwa aanze na mboga za majani za spinachi au aina nyingine. Ulaji wa aina hii unamwezesha mtu kula kidogo vyakula vyenye wanga, sukari au mafuta ambavyo vinasababisha kuongezeka uzito na unene. Saladi ya mboga za majani hujaza tumbo na kumfanya mtu ajihisi ameshiba na hivyo kuzuia tabia ya kutamani kula hasa vyakula vya wanga au sukari. Mboga za majani za spinachi pia, zina kirutubisho kinachoitwa thylakoids, ambacho kinachochea mwili kuzalisha homoni inayopunguza hamu ya mtu kutaka kula hasa vyakula vyenye sukari. Kuhusu matunda ya apple, kwa siku mtu akila tunda moja ni jambo zuri. Matunda ya apple yana maji na nyuzi lishe ambazo zinalifanya tumbo kujisikia limeshiba. Matunda ya epo pia yana kirutubisho cha pectin, ambacho kinakifanya chakula kilichomo tumboni kusagwa...