Ujasiri Wa Kukopa Ndio Utakaoboresha Biashara na Maisha Yako’
TAKWIMU zinaonesha kuwa Watanzania wengi hawaendi kukopa benki licha ya kuwapo kwa fursa hiyo. Sote tunafahamu kuwa benki ni wafanyabiashara kama walivyo wengine, wanauza na kununua fedha hivyo hiyo ndiyo bidhaa yao wanayoitegemea. Hivyo, kama ni wafanyabiashara wanachotazamia ni kupata faida kama ilivyo kwa wengine. Kukopesha ni huduma wanayotoa kati ya huduma zingine nyingi walizo nazo na hivyo lazima kupata faida. Sababu kubwa inayotajwa na watu ambao hawapendi kukopa benki ni kwamba wanadai masharti yao ni magumu, kuogopa kufilisiwa mali, riba kubwa na mlolongo mrefu wa kufuata taratibu ambazo zitamuwezesha mtu kukidhi vigezo vya kupata mkopo. Wengine wanasema biashara zao si za kijasiriamali hivyo zinauwezekano mkubwa wa kufa hatimaye kushindwa kulipa deni. Lakini pia, wengine wamekuwa wakikurupuka kukopa bila kupanga mipango madhubuti ya jinsi ya kurudisha – watu wanakopa ili kutatua matatizo yanayowakabili na si kuendeleza biashara zao. Kwa kutambua umuhimu wa mikop...