Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Aliyekimbia mgomo wa madaktari ajifungua watoto 5

Aliyekimbia mgomo wa madaktari ajifungua watoto 5

Picha
Moshi.  Raia wa Kenya, Bahati Tabu (37) amejifungua watoto watano mjini hapa Mkoa wa Kilimanjaro alikokimbilia kupata msaada kutokana na mgomo wa madaktari na wauguzi unaoendelea nchini humo. Mgomo huo unaohusisha madaktari na wauguzi zaidi ya 5,000 wa hospitali za Serikali, ulianza Desemba 6, mwaka huu na kudaiwa kusababisha zaidi ya wagonjwa 40 kupoteza maisha. Hata hivyo, watoto wanne kati ya hao walifariki dunia kwa kufuatana kila walipozaliwa katika Kituo cha Afya cha Faraja Himo. Akizungumza na gazeti hili kituoni hapo jana, mzazi huyo alisema huo ulikuwa ni uzao wake wa 11 na tayari ana watoto 10, miongoni mwa hao kuna mapacha. Aeleza alivyokimbilia Tanzania Bahati alisema alishindwa kwenda hospitalini nchini kwao kutokana na mgomo wa madaktari na wauguzi unaoendelea kushinikiza nyongeza ya mishahara na mazingira bora ya kazi. “Baada ya kuanza kuumwa uchungu, majirani walinichukua na kunileta Tanzania kujifungua na nilipofika hapa (Himo) nilikuwa tayari nakaribi...