Mabasi ya Mwendo Kasi ‘Yawatema’ Askari na Walimu
HUDUMA ya usafiri wa mabasi yaendayo haraka imeanza rasmi jana jijini Dar es Salaam huku yakilalamikiwa na watumiaji wakiwemo baadhi ya watu waliokuwa na msamaha wa kusafiri bila kutoa nauli, ambao sasa hawatambuliwi na mfumo mpya. Utaratibu uliokuwa umezoeleka awali wa askari wa polisi, jeshi, magereza na walimu kutolipa nauli kwenye usafiri wa daladala, umeonekana kugonga mwamba chini ya mabasi hayo. HabariLeo ilishuhudia mwalimu ambaye alikataa kutaja jina lake akitaka mwongozo wa kutolipa nauli kwa kuwa yeye ni mwalimu. “ Mama mfumo huu haumtambui mwalimu, askari,” alimjibu mmoja wa wahudumu wa UDA-RT aliyekuwa akihakiki tiketi za abiria kabla ya kupanda basi. Akijibu hoja hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa UDA-RT, David Mgwasa alisema mwongozo uliotolewa na Sumatra, unamtambua mwanafunzi pekee ambaye anatakiwa kulipa Sh 200, wengine wote wanatakiwa kulipa nauli. Mbali na walimu, askari, pia watu wenye ulemavu ambao walikuwa hawalipi nauli kwenye daladala, kwenye mfumo wa mabasi ya...