Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Serikali Yaupokea Ushauri wa Zitto Kabwe....Yaahidi Kuufanyia Kazi

Serikali Yaupokea Ushauri wa Zitto Kabwe....Yaahidi Kuufanyia Kazi

Picha
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali imepokea ushauri uliotolewa na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT- Wazalendo) wa kuishitaki Benki ya Standard (ICBC) ya Uingereza, kuhusu ufisadi uliofanyika katika mkopo wa Dola za Marekani milioni 600 (Sh trilioni 1.2) ambazo Serikali ilikopa kwa kutumia hati fungani. Ushauri mwingine uliotolewa na Zitto ambao Waziri Mkuu amesema Serikali itaufanyia kazi ni kuhusu Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), kuwafikisha mahakamani wahusika wa sakata la akaunti ya Tegeta Escrow, ili sheria ichukue mkondo wake. Zitto alitoa ushauri huo bungeni mjini Dodoma juzi, wakati akichangia hotuba ya bajeti ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, iliyowasilishwa na Waziri Angela Kairuki. Hotuba ya bajeti ya ofisi hiyo inajadiliwa na wabunge pamoja na ile ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), iliyowasilishwa na Waziri wake, George Simbachawene. Akizungumza na wanahabar...