Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Maya: Naitamani sana ndoa  na watoto wawili tu

Maya: Naitamani sana ndoa  na watoto wawili tu!

Picha
Staa wa ‘long time’ kwenye tasnia ya filamu Bongo, Mayasa Mrisho ‘Maya’. Kama kawa, kama dawa! Wiki hii tunaye mwanadada wa ‘long time’ kwenye tasnia ya filamu Bongo. Wengi wanamjua kwa jina la Maya lakini jina lake kamili ni Mayasa Mrisho. Paparazi wetu, Hamida Hassan alikutana naye kitaani na kumbana kwa maswali 10. Natumaini una hamu ya kujua kaulizwa maswali gani na yeye akayajibu vipi, kama jibu ni ndiyo, ungana nami hapa chini… Ijumaa: Mambo mdada, siku hizi umepotea kweli, tatizo nini mamy au umeolewa? Maya: Mh! Una maneno wewe, niko bize na mambo ya biashara ndiyo maana. Kwa filamu sifanyi kivile, nafanya kidogo kisha naendelea na mishe za kusaka noti. Ijumaa: Unadhani ni kwa nini soko la filamu kwa sasa limekuwa gumu kiasi cha kila mtu kusema mambo siyo mambo? Maya: Ni kweli soko limekuwa gumu, sababu ni wizi tunaofanyiwa, filamu feki zipo kibao mtaani, ukitoa filamu yako ikakulipa shukuru Mungu. Ijumaa: Vipi suala la kuwa na fa...