Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya MISIMU 17 VPL

MISIMU 17 VPL, MTIBWA SUGAR ITAENDELEA KUMPA NAFASI SHAABAN NDITTI

Picha
Na Baraka Mbolembole Shaaban nditti anamaliza msimu wake wa 17 mfululizo katika ligi kuu Tanzania bara na mchezaji huyo wa zamani wa Taifa Stars bado ana nguvu, maarifa, mbinu, na uwezo wa kupambana bila kuchoka na wachezaji vijana. Wakati wengi ‘wameingia na kutoka’ katika ligi kuu bara, Nditti amedumu tangu mwaka 1999 alikoanza soka lake akiwa na timu ya Singida United ya Singida. Alisajiliwa na Mtibwa Sugar kwa mara ya kwanza mara baada ya Mtibwa kutwaa ubingwa wao wa pili mfululizo wa VPL mwishoni mwa 2000. “Na bado kama Mungu anampa uzima basi atafikisha miaka 25 maana bado mwenye nguvu na anawajibika ipasavyo, na pia ana jitunza haswa”, anasema Yusuph Mgwao mshambuliaji wa zamani wa Simba SC na Mtibwa ambaye amewahi kucheza na Nditti katika timu zote hizo miaka ya 2004 na 2005. Nditti aliondoka Mtibwa na kusajiliwa na Simba mwishoni mwa mwaka 2003 lakini alishindwa kutulia klabuni hapo na baada ya kumalizika kwa msimu wa 2004 akaamua kurejea Mtib...