Serikali Yashauriwa Kuwa na Hisa Kwenye Kampuni za Madini ili Kujua Mapato halisi Yanayoingizwa na Wawekezaji wa Kigen
Serikali imeshauriwa kuwa na sehemu ya umiliki katika kampuni zinazochimba madini na gesi ili kujua mapato halisi yanayoingizwa na wawekezaji wa kigeni. Aidha, imeshauriwa kuzilazimisha kampuni hizo kurejesha nchini asilimia 60 ya mauzo yake, ili kuwa na akiba ya kutosha ya fedha za kigeni, pamoja na kuimarisha Shilingi ya Tanzania. Ushauri huo ulitolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali aliyestaafu, Ludovick Utouh pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Uhamasishaji wa Uwazi katika mapato ya Madini, Gesi na Mafuta (EITI), Jaji mstaafu Mark Bomani, wakati wa uzinduzi wa ripoti za kamati za mwaka 2013 na 2014 uliofanyika jana Dar es Salaam. Akizindua ripoti hizo, Utouh alisema, Tanzania haijafaidika na rasilimali za madini, jambo lililosababishwa na kujiondoa kufanya biashara, hivyo kuzipa mwanya kampuni za kigeni kuendesha biashara bila uwazi kuhusu mapato zinazoyapata kutokana na mauzo ya madini. “ Serikali iliangalie jambo hili na kulirekebisha, Serikali ya...