Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Kambi Rasmi ya Upinzani Yapinga Tabia Ya Kutumbua Majipu Inayofanywa na Serikali ya Rais Magufuli

Kambi Rasmi ya Upinzani Yapinga Tabia Ya Kutumbua Majipu Inayofanywa na Serikali ya Rais Magufuli

Picha
KAMBI Rasmi ya Upinzani imepinga tabia ya ‘kutumbua majipu’ inayofanywa na serikali ya Dk John Magufuli hivyo imewataka watumishi na watendaji wa umma waliosimamishwa au kufukuzwa kazi na mawaziri, kufungua mashauri Mahakama Kuu ya Tanzania ili kupinga kufukuzwa kwao na baadhi ya mawaziri. Hayo yamesemwa leo katika hotuba ya maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani kuhusu Mpango na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa Mwaka wa Fedha wa 2016/2017. Kwa mujibu wa hotuba hiyo, Lissu amesema kuwa baadhi ya mawaziri waliosimamisha na au kufukuza kazi watumishi wa umma kwa jina maarufu kutumbua majipu, walifanya maamuzi hayo kinyume cha sheria. Ameongeza kuwa Mawaziri hao hawakuwa na mamlaka ya kufanya hivyo kwa sababu hawajakasimishwa mamlaka ya utekekelezaji wa majukumu yao kwa mujibu wa kifungu cha sheria cha 5(1) cha utekelezaji wa majukumu ya kiuwaziri. Kutokana na hali hiyo kambi ya upinzani imesema watumishi wote ambao wametumbuliwa wana haki na uwe...