Serikali yawakalia Kooni Watumishi wazembe na wabadhilifu
Serikali imesema kuanzia sasa mtumishi wa umma atakayeshindwa kusimamia rasilimali za umma, achague moja kati ya mawili, kuacha kazi au atumbuliwe. Hayo yalisemwa jana na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango wakati alipozindua kitabu cha mwongozo wa usimamizi wa rasilimali za umma unaolenga kuhakikisha miradi ya maendeleo inatekelezwa na kusimamiwa vizuri kwa maslahi ya Taifa. Dk Mpango alizindua kitabu hicho jana katika ukumbi wa Hazina mjini Dodoma na baadaye semina elekezi iliyoandaliwa na Tume ya Mipango ilitolewa kwa watumishi wa Serikali. Akizindua kitabu hicho, Dk Mpango alisisitiza kuwa mtumishi atakayeshindwa kuendana na maelekezo hayo ‘atatumbuliwa’. “Mkishindwa kusimamia miradi kuna mawili, muache kazi mapema kama hamuwezi usimamizi au tuwatumbue, katika hilo hatutasita,” alisema Katika ufafanuzi wake, Dk Mpango alisema katika bajeti ya Serikali mwaka 2016/17, fedha za maendeleo zilizotengwa ni asilimia 40 ya bajeti yote, hivyo lazima iw...