Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Genes Shayo anashikiliwa na Kikosi cha kupambana na ujangili kwa tuhuma za kujihusisha na ujangili.

Mhifadhi Mwandamizi wa TANAPA, Genes Shayo anashikiliwa na Kikosi cha kupambana na ujangili kwa tuhuma za kujihusisha na ujangili.

Picha
Vita dhidi ya ujangili inazidi kushika kasi baada ya kikosi kazi maalumu cha kupambana na ujangili kumnasa Mhifadhi Mwandamizi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa) kwa tuhuma za ujangili. Pia, kikosi hicho kimemtia mbaroni Mchungaji wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG), wilayani Arumeru kwa tuhuma za kukutwa na jino la tembo wakati akisaka mnunuzi. Waziri wa Utalii na Maliasili, Profesa Jumanne Maghembe alisema jana kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vimeongeza kasi ya kupambana na majangili katika mapori yote ya akiba. Meneja Uhusiano wa Tanapa, Paschal Shelutete katika taarifa yake jana alisema kuwa Mei 14, mwaka huu, shirika hilo lilipokea taarifa za siri kuwa mchungaji huyo alikuwa akimiliki jino hilo. “Tuliambiwa mchungaji huyo alikuwa akihitaji mtu wa kufanya naye biashara. Baada ya kupata taarifa tuliwasiliana na kikosi kazi maalumu cha kitaifa ili wafuatilie,”  alisema Shelutete. Shelutete alidai kuwa Mei 15, mchungaji huyo alikamatwa na kumtaj...