Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Jaji Warioba Azungumzia Uchaguzi Mkuu wa 2015

Jaji Warioba Azungumzia Uchaguzi Mkuu wa 2015

Picha
Waziri Mkuu mstaafu, Joseph Warioba amesema Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana (2015) ulifanyika kwa haki huku akitaka vyama vya siasa kuwa na demokrasia ndani yao, kuhakikisha wanayotaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) iwafanyie, wao pia wayafanye kwenye vyama vyao. Amesema nchi inatakiwa kuangalia na kujadili uchaguzi usiwe bidhaa inayotafutwa kwa fedha kama ambavyo ilijitokeza katika uchaguzi wa mwaka jana ambao rushwa ilitumika kwa kiwango kikubwa. Akizungumza katika mdahalo wa kitaifa kuhusu uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka jana, Warioba pia ametoa angalizo kwa asasi za kiraia kuwa makini na wafadhili wao kuepuka kuingiza matakwa yao (wafadhili) kwenye siasa za ndani. Mdahalo huo uliofanyika jana jijini Dar es Salaam, ulioandaliwa na Mpango wa Elimu ya Demokrasia Tanzania (REDET) na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, (LHRC). Akiwasilisha mada, Warioba ambaye amepongeza utendaji wa Rais John Magufuli, alisema uchaguzi mkuu ulikuwa na hamasa ambayo haijapata kutokea lakini ulikuwa ...