Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Bush Asema Hatampigia Kura Donald Trump

Bush Asema Hatampigia Kura Donald Trump

Picha
Aliyekuwa mgombea wa urais wa tiketi ya chama cha Republican nchini Marekani, Jeb Bush amesema hatampigia kura Donald Trump katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika nchini humo Novemba mwaka huu. Bush alisema kuwa Trump hana tabia wala mienendo ya kuwa Rais wa Marekani. ‘‘Marais wa Marekani wanasifa zao na wanakubalika kwa watu, lakini huyu jamaa hana sifa hata moja ndiyo maana kila siku namkana na kusema hafai kabisa kuwa rais wa nchi hii, ’’alisema Bush Jeb ni mojawapo wa wanachama mashuhuri wa Republican kutanganza hadharani kuwa hatampigia kura Trump kwa sababu ya kampeni yake ya kiburi ambayo imegawanya Chama cha Republican. Juzi Spika wa Bunge, Paul Ryan alisema hatamuunga mkono mfanyabiashara huyo tajiri ingawa atakutana naye wiki ijayo. Hata hivyo, Trump aliungwa mkono na mgombea urais wa zamani wa nchi hiyo, Bob Dole aliyeshindwa katika uchaguzi na Bill Clinton wa Chama cha Democratic mwaka 1996. Wiki iliyopita Seneta wa Texas, Ted Cruz alijitoa katika...