Hatifungani "BOND" Ya Benki ya NMB Kuwainua Wananchi Kiuchumi
NMB imeanza kupita kila kona kutoa elimu kwa wananchi na wafanyabiashara kuhusu uwekezaji wa fedha kupitia BOND “Hati fungani”. Hati Fungani ni namna moja wapo ya kumpa mwananchi njia mbadala ya kuwekeza pesa zake na kuachana na “vibubu”. Akiongea na waandishi wa habari, Meneja Mawasiliano Mwandamizi wa NMB Bi. Joseline Kamuhanda alisema Hati Fungani ni njia moja wapo ya kuwasaidia wananchi kuachana na tabia ya kuweka pesa zao ndani bila faida yoyote. “Hati Fungani inampa mwananchi njia mbadala ya uwekezaji wa pesa, fedha utayoiwekeza itakupa faida zaidi kulingana na kiasi cha hati fungani zilizonunuliwa.” alisema. Ili kuweza kuwekeza pesa zako kupitia hati fungani unahitaji kuwa na Central Depository System (CDS account) ambayo inatolewa na Soko la Hisa la Dar es Salaam. Namba hii hutunza kumbukumbu za mteja katika Soko la Hisa na pia hutumika katika kununua na kuuza hisa. Meneja wa mahus...