SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 28 Aprili 2016

T media news

Hatifungani "BOND" Ya Benki ya NMB Kuwainua Wananchi Kiuchumi


NMB imeanza kupita kila kona kutoa elimu kwa wananchi na wafanyabiashara kuhusu uwekezaji wa fedha kupitia BOND “Hati fungani”. 

Hati Fungani ni namna moja wapo ya kumpa mwananchi njia mbadala ya kuwekeza pesa zake na kuachana na “vibubu”.

 

Akiongea na waandishi wa habari, Meneja Mawasiliano Mwandamizi wa NMB Bi. Joseline Kamuhanda alisema Hati Fungani ni njia moja wapo ya kuwasaidia wananchi kuachana na tabia ya kuweka pesa zao ndani  bila faida yoyote.

 

“Hati Fungani inampa mwananchi njia mbadala ya uwekezaji wa pesa, fedha utayoiwekeza itakupa faida zaidi kulingana na kiasi cha hati fungani zilizonunuliwa.” alisema.

 

Ili kuweza kuwekeza pesa zako kupitia hati fungani unahitaji kuwa na Central Depository System (CDS account) ambayo inatolewa na Soko la Hisa la Dar es Salaam. Namba hii hutunza kumbukumbu za mteja katika Soko la Hisa na pia hutumika katika kununua na kuuza hisa. 

 

Meneja wa mahusiano ya wawekezaji Bi. Anna Mwasha, akizungumza na waandishi wa habari alisema uwekezaji kupitia hati fungani utawanufaisha wananchi wote ambao  licha ya kutumia nguvu na rasilimali nyingi, hawapati faida wanayostahili kutokana na tabia ya kuwekeza pesa zao kwenye vitegauchumi visivyo na faida ya uhakika.

 

“Ni kitu kizuri kwa kuwa ukiwekeza kwenye hati fungani,  hata utapokuwa unataka pesa yako kabla ya muda wa ukomavu, unaweza kuuza hati fungani hiyo kwenye Soko la Hisa na badala yake, mwananchi mwingine ataendelea kupokea riba mpaka muda wa ukomavu wa hati fungani, hivyo ni kitu ambacho ni kizuri kwa kila mtu”. Alisema Meneja wa mahusiano ya wawekezaji