SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 28 Aprili 2016

T media news

Nyota yazidi kungaa kwa Donald Trump USA

   

         

Mchakato wa kumpata mgombea wa urais katika vyama vya Republican na Democratic nchini Marekani unazidi kushika hatamu huku nyota njema ikizidi kuoneakana kwa Mgombea Donald Trump wa chama chama cha Republican.

Hii ni baada ya ya Trump kushinda mchujo wa uteuzi katika uchaguzi wa chama cha Republican kwenye majimbo matano uliofanyika jumanne hii, majimbo amabayo ameshinda mchujo wa kuteua mgombea urais ni Connecticut, Delaware, Maryland, Pennsylvania na Rhode Island.

Licha ya ushindi huo Donald Trump anakumbwa na upinzani mkubwa sana kutoka kwa baadhi ya wanaharakati ndani na nje ya Marekani, hii ni kutokana na sera zake zinazochukuliwa kama ni za kibaguzi, mojawapo ya sera zake ni ile ya kujenga ukuta kwenye mpaka wa Marekani na Mexico.

Trump bado ameendelea kushikilia sera zake na aliwaambia wafuasi wake New York kwamba hatabadilisha sera zake iwapo atachaguliwa kuwa rais.

"Sibadiliki, Mnafahamu kwamba nilisomea shule bora zaidi. Mimi ni mtu mwerevu sana. Nitaiwakilisha nchi hii kwa heshima na vyema sana. Lakini sitaki kubadilisha sifa zangu binafsi. Mnajua, ndizo zilizonifikisha hapa.” Alisema.

Ushindi huo wa Jumanne unamfanya bwana Trump kukaribia kutimiza idadi ya wajumbe wanaohitajika ili kuweza kuteuliwa kupeperusha bendera ya chama cha Republican katika uchaguzi mkuu wa urais. Hatua hiyo imemfanya Trump kutembea kifua mbele na kujitangaza kuwa yeye ni ‘‘mgombea mteule’’ wa Republican.

Wakati mambo yakiwa shwari kwa Trump upande wa pili wa Democratic mambo yaliemuendea kombo Bi Hilary Clinton. Baada ya kushindwa na mgombea mwenzie wa Democratic Bwana Bernie Sanders  katika jimbo la Rhode Island.

Katika ukumbi wa mkutano wa Philadelphia ambapo Bi Clinton alitangazwa mshindi wa majimbo manne kati ya matano amesema kuwa kampeni yake inaweka “malengo jasiri na ya kupiga hatua mbele” katika kuimarisha maisha ya watu Marekani.

“Sisi tunaamini katika wema wa watu wetu na ukuu wa taifa letu,” alisema Bi Clinton.