Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Salama Jabir

Salama Jabir, binti asiyecheza na maswali

Picha
Kama upo Afrika Mashariki na Kati bila shaka jina la Salama Jabir si geni kwako. Binti mdogo mdogo kwa umbo ila mahojiano yake katika kipindi chake maarufu cha Mkasi kinachorushwa kutoka Tanzania huwa na maswali ya kiuchokozi sana. Pia ni mmoja wa majaji katika mashindano ya kutafuta wenye vipaji vya kuimba yaani Bongo Star Search. Alitutembelea hivi karibuni hapa katika studio zetu, na mwanzo Zuhura Yunus alitaka kujua ni rahisi kiasi gani kufungua kampuni yako mwenyewe ukizingatia yeye amejiajiri.