Video: Chid Benz Adaiwa Kutoroka Sober House
Wakati wadau wa muziki wakifahamu kuwa Msanii wa Muziki wa Hip Hop Bongo, Rashid Makwilo ‘Chid Benz’ yuko katika kituo cha kusaidia waathirika wa madawa ya kulevya ‘sober house’ kilichopo Bagamoyo mkoani Pwani, inadaiwa jamaa alishatoroka kitambo na sasa yuko kitaa. Taarifa iliyotua kwenye meza ya dawati hili ilidai kuwa, Chid alitoroka kituoni hapo baada ya kushindwa kuhimili mazingira yalikuwepo hivyo akaona bora arudi mtaani kwa staili ya liwalo na liwe. Baada ya kupata taarifa hiyo, mwishoni mwa wiki iliyopita waandishi wetu walitinga Bagamoyo na kukutana na meneja wa kituo hicho, Tumaini Majura ambaye alithibitisha kuondoka kwa Chid akiwa bado anaendelea kupatiwa matibabu. Sehemu ya mahojiano kati ya Risasi na meneja huyo ni hii; Chid-Beenz_fullRisasi: Kwani Chid Benz ameishi hapa kwa muda gani? Tumaini: Ni siku 28 lakini alitakiwa kukaa kwa muda wa angalau miezi mitatu ili kurudi katika hali yake ya kawaida. Risasi: Ilikuwaje sasa mpaka akaondo...